Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa takriban wanajeshi 900 wa Ukraine wameuawa katika operesheni zilizofanywa na jeshi la Russia kwenye maeneo mbalimbali ya Ukraine.
Wiki iliyopita pia, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kwamba wakati wa operesheni za kijeshi huko Donetsk, Krasnolimansk na Kobyansk, vikosi vya jeshi la nchi hiyo vilizuia mashambulizi 13 ya jeshi la Ukraine na kuua wanajeshi 705 wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema kwamba, jeshi la nchi hiyo limeimarisha nafasi yake katika maeneo ya Donetsk kusini mwa Ukraine, Kup’yans’k katika mkoa wa Kharkiv , Donetsk, Krasny Limansk na Zaporozhye, na kwamba vikosi vya jeshi la Russia vimezima mashambulizi kumi na moja ya Ukraine na kuua wanajeshi 890 wa nchi hiyo.
Russia pia imetangaza kuwa, imeharibu kabisa vituo viwili vya kurushia ndege zisizo na rubani vya Ukraine huko Lastochkyne, Donetsk na Ivanovskoye katika mkoa wa Zaporozhye, na vilevile kituo cha uongozi cha Brigedi ya 67 na ghala la silaha karibu na mkoa wa Serebrianka huko Donetsk.
Ndege zisizo na rubani 18 za Ukraine pia zimetunguliwa.
Seymour Hersh, mwandishi mashuhuri wa habari za uchunguzi wa Marekani, hivi karibuni alisema kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lilikuwa tayari limemuonya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Anthony Blinken kuhusu kufeli kwa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Russia.