Takriban watu 10 wameuawa baada ya paa la kanisa kuporomoka kaskazini mwa Mexico, maafisa wa eneo hilo wanasema.
Watu 49 walipelekwa hospitali baada ya kuporomoka kwa kanisa la Santa Cruz katika mji wa pwani wa Ciudad Madero katika jimbo la Tamaulipas.
Takriban watoto wawili wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waliouawa.
Watu 60 walitibiwa majeraha, gavana huyo alisema, huku 23 wakiwa bado wamelazwa hospitalini.
“Wawili wana majeraha mabaya, maisha yao yanaweza kuwa hatarini,” alisema.
Takriban watu 100 walikuwa wakihudhuria Misa wakati huo, polisi walisema. Baadhi ya ripoti zilidokeza kwamba sherehe ya ubatizo ilikuwa ikifanywa huko.
Makumi ya watu waliachwa wamenasa ndani ya kanisa kufuatia tukio hilo. Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha jengo la kanisa likiwa magofu huku watu wakijaa kuzunguka vifusi, wakiwasaka waliopotea.
Gavana wa Tamaulipas, Américo Villarreal, baadaye alisema kwamba wote waliopotea wamehesabiwa, kulingana na shirika la habari la Agence France-Presse (AFP).
“Kanisa lilikuwa limejaa watu wapatao 100, na watu walikuwa wamejipanga ili kuchukua ushirika – bila shaka hiyo ni aina ya kilele cha Misa ya Kikatoliki – na hapo ndipo paa ilipoanguka juu yao; matofali, saruji, na miundo ya msaada wa chuma ikishuka juu ya watu,” alisema.