Takriban watu watatu waliuawa katika shambulio la usiku la Urusi la kombora dhidi ya Ukraine, na wa nne aliuawa kwa kupigwa makombora Jumatatu asubuhi, maafisa wa Ukraine walisema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Ihor Klymenko alisema watu watatu waliouawa walikuwa wafanyakazi katika kituo cha viwanda katika eneo la Poltava. Wengine watano pia walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo, na mtu mwingine hajulikani aliko.
Gavana wa eneo la Kherson, Oleksandr Prokudin, alisema mwanamke mwenye umri wa miaka 63 aliuawa katika shambulio la makombora katika kijiji cha Sadove Jumatatu asubuhi.
kwingineko ,shirika la habari la Urusi Tass liliripoti kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi ilidungua ndege mbili zisizo na rubani katika eneo la Crimea.
“Leo, karibu 10:30, jaribio lingine la serikali ya Kyiv kufanya shambulio la kigaidi la UAV mbili za aina ya ndege kwenye vitu katika Shirikisho la Urusi lilizimwa.
Magari mawili ya anga ambayo hayakuwa na rubani yaliharibiwa na vikosi vya ulinzi wa anga vilivyokuwa kazini katika eneo la Jamhuri ya Crimea,” Tass alinukuu wizara ya ulinzi akisema. Mkuu wa eneo hilo, Sergey Aksyonov, aliongeza kwenye Telegram kwamba ndege mbili zisizo na rubani za upelelezi zilidunguliwa kaskazini na magharibi mwa Crimea.