Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR, limesema takriban watu laki moja na nusu wamekimbia kutoka Ukraine kuingia katika mataifa jirani kutafuta usalama wakati Urusi ikishambulia mji mkuu wa nchi hiyo pamoja na miji mingine.
Msemaji wa shirika hilo Shabia Mantoo, amesema kuwa takriban watu 116,000 wamevuka mipaka ya kimataifa na idadi hiyo inaoongezeka kila dakika.
Shirika hilo la kuwashughulikia wakimbizi, linakadiria kuwa huenda takriban raia milioni 4 wa Ukraine wakatoroka nchi hiyo iwapo hali itaendelea kuwa mbaya zaidi.
Mantoo anasema raia wengi wanakimbilia katika mataifa jirani ya Poland, Moldova, Hungary, Romania na Slovakia, huku wengine wakikimbilia Belarus.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameazimia kuongeza msaada wa kibinadamu kwa Ukraine kutokana na uvamizi wa Urusi