Mwanafunzi mmoja amefyatua risasi katika chuo kikuu cha Prague, na kuua takriban watu 14, na kujeruhi zaidi ya 20 katika shambulio baya zaidi la watu wengi katika Jamhuri ya Czech maafisa walisema.
Umwagikaji huo wa damu ulifanyika katika jengo la idara ya falsafa ya Chuo Kikuu cha Charles, ambapo mpiga risasi alikuwa mwanafunzi, Mkuu wa Polisi wa Prague Martin Vondrasek alisema. Mshambuliaji huyo pia alikufa, mamlaka ilisema na Jina lake halijatolewa.
Vondrasek alisema alhamis jioni kwamba watu 14 walikufa na 25 walijeruhiwa, baada ya kuripoti mapema kuwa 15 walikufa na 24 walijeruhiwa. Hakueleza mabadiliko. Mamlaka zilionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
Polisi hawakutoa maelezo yoyote kuhusu waathiriwa au sababu inayowezekana ya ufyatuaji risasi kwenye jengo lililo karibu na Mto Vltava katika uwanja wa Jan Palach. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Czech Vit Rakusan alisema wachunguzi hawashuku kuwa kuna uhusiano na itikadi kali au vikundi vyovyote vya itikadi kali.
Vondrasek alisema polisi wanaamini kuwa mtu mwenye bunduki alimuua babake mapema Alhamisi katika mji alikozaliwa wa Hostoun, magharibi mwa Prague, na kwamba pia alikuwa akipanga kujiua. Hakufafanua.
Baadaye Alhamisi, Vondrasek alisema kwamba kulingana na upekuzi katika nyumba yake, mtu mwenye bunduki pia alishukiwa katika mauaji ya mwanamume mwingine na bintiye wa miezi 2 Desemba 15, huko Prague.
Chifu huyo alimtaja mpiga risasi huyo kama mwanafunzi bora asiye na rekodi ya uhalifu, lakini hakutoa taarifa nyingine yoyote.
Mshambuliaji huyo alipata majeraha mabaya lakini haikuwa wazi ikiwa alijiua au alipigwa risasi hadi kufa katika majibizano ya risasi na maafisa, Vondrasek alisema, na kuongeza kuwa hakuna chochote cha kupendekeza kwamba alikuwa na mshirika.
Mshambuliaji huyo alimiliki bunduki kadhaa kihalali polisi walisema alikuwa na silaha nyingi Alhamisi na alikuwa amebeba risasi nyingi na kwamba alichokifanya “kilifikiriwa vyema, kitendo cha kutisha,” Vondrasek alisema.
Mamlaka ya chuo kikuu ilisema itaimarisha usalama katika majengo ya chuo kikuu mara moja.