Shirika la Kitaifa la Zimamoto la Taiwan (NFA) lilisema katika sasisho Alhamisi kwamba watu 663 wamesalia wamekwama kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba kaunti ya kaskazini ya kisiwa hicho cha Hualien.
Idadi ya vifo imesalia kufikia tisa, na watu 1,067 wamejeruhiwa, kulingana na shirika hilo.
Siku ya Jumatano, zaidi ya watu 200 walikuwa kwenye makazi katika Kaunti ya Hualien na kaya 10,000 hazikuwa na maji.
Makumi ya watu pia walinaswa kwenye migodi kote kanda siku ya Jumatano.
Watu 64 walinaswa kwenye mgodi wa shimo wazi wa Heping huko Hualian. NFA ilisema wote walihamishwa wakiwa salama karibu Alhamisi adhuhuri.
Watu saba walinaswa katika mgodi wa Zhonghe. NFA ilisema watu sita waliokolewa kutoka kwa mgodi huo ulioko kwenye machimbo.