Rais John Magufuli ameziagiza Mamlaka zinazohusika, kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo jijini DSM wakati akizindua karakana kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hata hivyo Rais Magufuli amesisitiza kuwa Virusi vya Corona havijaingia nchini, lakini tahadhari ni muhimu.
“Elimu itolewe kuhusu corona, Wanahabari ikiwezekana kila siku Mhariri atoea tahadhari ya corona, hata kabla ya taarifa ya habari, tutoe elimu mashuleni, vyuoni, hata kwenye daladala makondakta watoe elimu kwa abiria,Viongozi tutoe elimu mikoani, Viongozi wa Dini tuombe sana”.