Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 imeeleza kuwa taarifa za kifedha za shirika la umeme Tanzania (TANESCO) za Mwaka 2019/20 zimebainisha kuwa, Shirika lina mtaji hasi wa uendeshaji (Negative Working Capital) wa Shilingi Trilioni 1.33.
Shirika kuwa na mtaji hasi kumetokana na mali za muda mfupi za Shirika za kiasi cha Shillingi Trilioni 1.45 kushindwa kulipa madeni ya muda mfupi ya kiasi cha Shilingi Trilioni 2.78.
Uwezekano wa hali hii kuendelea ni mkubwa sana kutokana na utendaji wa Shirika kuwa na madeni mengi ya haraka (current liabilities) ikilinganishwa na mali zilizopo. Kamati imeshauri Shirika kuwa na Mpango wa Biashara ambao utaainisha kiasi cha mtaji kinachohitajika.