Mwananchi mmoja mkazi wa mwamboni mkoani Tanga amelipwa kiasi cha shilingi 778,000 kama fidia mara baada ya kuunguliwa na vitu vyake vya ndani kutokana na hitilafu ya umeme ulio sababishwa na waya wa umeme kukatika na kudondokea nyumba yake.
Akizungumza na millardayo.com na Ayotv mwananchi huyo aliefahamika kwajina la Mwamvua Maliki alisema kuwa mnamo majira ya saa kumi na moja jioni ndipo walipo sikia shoti ya umeme na wao kukimbia nyumbani ili kuokoa Maisha yao.
“tulisikia shoti ya umeme kwa mara ya kwanza tukakimbia baadaye kidogo mara baada ya kupoa tukarudi ila tulivyo rudi ndio tulio sikia mlio mkubwa wa shoti ndio ikabidi tukimbie wote majirani ndio waliona moto mkubwa una waka kutoka kwenye mita ndipo vijana wakajitolea kuuza nafsi zao kwa kuja kuzima moto huo kwa maji’’
“mara baada ya zima moto kuja na kufanikia kuzima moto huo tanesco walitaka kuondoka tukawafata na kuwaambia twendeni huku kuna shoti kubwa imetokea ndio wakaja kupiga picha na kunihoji maswali juu ya tukio hilo mara baada yahapo wakaondoka bila msaada wowote.’’ Alisema mwanamvua.
Aidha mwanamvua amebainisha kuwa alipata msaada kutoka kwenye kipindi cha radio kinachotolewa na EWURA CCC (Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma ya za Nishati na Maji) juu ya haki za mteja na fidia zinazo tolewa kwa mteja mwenye changamoto juu ya huduma za nishati na maji ndipo alipo pata msaada wa changamoto iliyokuwa inamkabili.
“mara baada ya kusikiliza kipindi cha radio niliweza kupata mawasiliano yao na hivyo nilifika ofisi kwao nikajaza fomu ya malalamiko kwaajili ya kudai fidia ya vitu vilivyo ungua baada ya hapo EWURA ili ili kuja na kunisikiliza mimi Pamoja na tanesco mara baada ya kikao cha usuluhishi ndipo EWURA ilikuja na muafaka wa tanesco kunilipa fidia ya kiasi cha shilingi 778,000’’Alisema Mwanamvua.
Kwaupande afisa huduma kwa wateja na utawala kutoka EWURA CCC Nuru Zuberi
Amekiri kumuhudumia mteja huyo na kumsaidia kuweza kupata haki yake ya msingi kwani ni moja kazi ya EWURA CCC katika kutoa huduma kwa kwa wananchi.
“mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mteja sisi kama EWURA CCC tulimjazisha fomu na kuipeleka EWURA kwa ajili ya kikao cha usuluhishi kilicho hitishwa na EWURA ikijumuisha mlalamikaji,mlalamikiwa Pamoja na ewura ccc mara baada ya kikao hicho EWURA ili mtaka tanesco kumlipa mlalamikaji kiasi cha tsh.778,000/= kama madai yake baada ya hasara alio ipata kutokana na shoti hiyo.’’