TanTrade imekuwa na jukumu utoaji taarifa za upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi, mathalan kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 jumla ya Kampuni 31,891 zilipatiwa taarifa mbalimbali za kibiashara kuhusu bei na masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Kati yao wafanyabiashara 405 waliweza kuunganishwa na masoko na kuuza tani 102,000 za mahindi, tani 2,000 za karanga, tani 5,000 za soya, tani 50 za ufuta, tani 7 za majani ya papai, kilogramu 200 za unga wa ubuyu, tani 2 za iliki, tani 5,000 za muhogo na tani 3.2 za tangawizi ya unga.
Miongoni mwa bidhaa zilizoonesha uhitaji mkubwa katika masoko ya nje ni pamoja na matunda, samaki na mazao ya bahari (mwani), jamii ya mikunde, asali, kahawa, chai, korosho, viungo na vyakula.
Maulizo hayo yalitoka katika nchi za India, Nchi za ukanda wa SADC, China, Japan, nchi jirani za Afrika Mashariki (EAC), Falme za Kiarabu, Misri, Marekani, Vietnam na Ulaya.