Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio amesema nchi inaweza kuwa katika hali ya hatari ikiwa meli yenye mafuta isipofika ndani ya siku 15 kwa kuwa mafuta yaliyopo yanatosha kwa siku 15 tu.
Dkt. Mataragio amesema bei ya mafuta kwenye Soko la Dunia imekuwa ikishuka lakini bei zimekuwa tofauti kwa Tanzania ambayo unafuu wa bei za mafuta hauonekani.
“Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda, hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu,” Dkt. Mataragio
Dk. Mataragio amesema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.
“Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia,” Dkt. Mataragio
MZEE ANAISHI NA MAMBA TANZANIA, ANAONGEA NAE KAMA MTOTO WAKE, ANAMUITA “AJABU”