Sekta ya Utalii nchini Tanzania inachangia Dola za Marekani Bilioni 2.6 katika uchumi wa nchi ikilinganishwa na Kenya ambako inachangia Dola za Marekani Bilioni 1.7 na kuifanya Tanzania iongoze kwa mapato yatokanayo na Utalii kwa nchi za Afrika Mashariki.
Takwimu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar zinaonesha kuongezeka kwa mapato ya Utalii kutokana na idadi kubwa ya Watalii wanaokuja nchini Tanzania kuona na kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii.
Kufuatia mchango huo Tanzania inashika nafasi ya pili kwa mapato yatokanayo na Utalii katika nchi 10 zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.