Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema wamekubaliana na Serikali ya Rwanda kufungua mpaka mpya wa kuingia Rwanda uliopo Kyerwa Mkoani Kagera.
Waziri Makamba ameyasema hayo mara baada ya Mkutano na Mawaziri wanne wa Sekta mbalimbali Rwanda kujadili na kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili ambazo zaidi likilengwa eneo la uwepo wa biashara kubwa kwa Tanzania na Rwanda.
Waziri Makamba amesema ‘Mwaka jana Rwanda ilikua Nchi ya tatu kwa matumizi ya Bandari yetu, Ni muhimu nchi yetu iendelee kupata biashara hiyo ya Rwanda, Tumekuja hapa ili kuzungumza na wenzetu ili kuona ni kiasi gani tunaweza kuongeza kiwango hiko cha biashara kati ya Tanzania na Rwanda kwenye matumizi ya bandari yetu’ – Makamba.
‘Nchi yetu (Tanzania) na Rwanda tuna mpaka mmoja tu rasmi wa Rusumo, kwa hiyo tumekubaliana kuwa tutafungua mpaka mwingine wa Kyerwa ili kurahisisha biashara na mahusiano ya Nchi zetu hizi mbili’ – Waziri Makamba.