Mamlaka ya usimamizi wa Uvuvi Bahari kuu Tanzania (DSFA) inatarajia kufunga vifaa vya kisasa zaid kwenye meli zinazovua kwenye bahari kuu ikiwemo meli za nje zilizosajiliwa Tanzania kwa shughuli za Uvuvi wa Bahari kuu kwa ajili ya kupata zaid mawasiliano yanayoendelea kwenye meli za uvivvu ambapo USAID imejitolea kuipa Tanzania Billion 627 kwa ajili ya ufungaji wa vifaa hivyo kwenye meli na kufunga mkataba na Tanzania wa miaka mitano
Msimamizi wa Mradi wa Heshimu Bahari wa USAID Mathiac Igulu amesema ni fedha nyingi ambazo imeipatia Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha kua kunakua na mazingira endelevu na rasilimali zake zinahifadhiwa kwa kufungw kwa vifaa hivyo kwenye meli za uvuvi wa bahari kuu ukanda wa kusini mwa Pwani ya Tanzania,ikiwemo Visiwa vya Unguja na Pemba
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usimamizi Uvuvi wa bahari kuu Dkt Emmanuel Andrew Sweke amesema camera hizo zinazofungwa ziatasaidia kupata matukio kwa usahihi wakati shughuli za uvuvi wa bahari kuu moja kwa moja zikiwa zinaendelea na itasaidia kutokuikwa masharti mbali mbali kama rasilimali endelevu ,uvuvi haramu na Biashara Haramu za Binadamu