Moja kati ya mipango ya Serikali kupitia kwa Waziri wa sanaa utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa ni kuona Tanzania inashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika Mwaka 2030.
“Ndoto yetu kama serikali mwaka 2030 tushiriki Fainali za Kombe la Dunia na nina amini inawezekana, tumeshatenga fedha [bajeti] kwa ajili ya kuboresha na kujesha viwanja vya kisasa, tunatumia chuo cha Malya kutoa mafunzo ya michezo kwa waamuzi, makocha na wataalam wengine.”
“Tumeandaa mchakato wa tafiti ambao chuo cha Malya watatuletea utafiti ni namna gani tunaweza kupiga hatua katika kushiriki mashindano mbalimbali ya kikataifa na ni kwa nini hatufanyi vizuri”