Tanzania na nchi jirani ya Rwanda inatarajiwa kufungua mpaka wa pili kati yao.
Makubaliano hayo yaliafikiwa mjini Kigali wakati wa mazungumzo kati ya mawaziri wa masuala ya kigeni kutoka nchi hizo mbili.
Akizungumza baada ya mkutano huo Waziri wa masuala ya kigeni wa Tanzania January Makamba alisisitiza kwamba Tanzania iko tayari kuimarisha ushirikiano na Rwanda kwa lengo la kuinua maisha ya raia wa mataifa hayo mawili kupitia biashara, teknolojia, viwanda na kawi.
Aidha Makamba amesema kwamba mpaka huo utawarahisishia raia wa mataifa hayo mawili kuvuka na kutembeleana.
Waziri Makamba amewahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa baadhi ya changamoto za usafirishaji na utoaji wa bidhaa kupitia Tanzania bado zinatafutiwa ufumbuzi.
Kabla ya kufanya mazungumzo na mwenzake, Waziri Makamba alitembelea Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari mjini Kigali.
Article share tools