Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia Bi Lillian Bwalya wamesaini nyaraka za makubaliano (Communique) ya changamoto za kibiashara kati ya Tanzania na Zambia zilizoondolewa na zile zilizobaki kutatuliwa kabla ya Novemba 30, 2023.
Makatibu Wakuu hao wamesaini nyaraka hizo za makubaliano (Communique) ya kutatua changamoto za kibiashara kati ya Tanzania na Zambia katika Mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu wakati wa Mkutano wa Pili wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika katika Mpaka wa Nakonde – Zambia Novemba 07, 2023
Vilevile Dkt. Abdallah amesema utatuzi wa Changamoto hizo utaiwezesha sekta binafsi kaika nchi zote mbili kufanya biashara kwa urahisi na tija hususani katika biashara ya huduma ya usafirishaji mizigo kutoka Tanzania kupitia Zambia na kwenda nchi nyingine na mizigo kutoka Zambia kupitia Tanzania kwenda nchi nyingine.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia Bi Lillian Bwalya amesema nchi hizo zitaendelea kushirikiana katika kitatua changamoto hizo pamoja na nyingine zitakazojitokeza ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa pande zote mbili.