Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma amesema kuwa Tanzania kwasasa inashikilia namba mbili miongoni mwa nchi zinazozalisha zao la Tumbaku Barani Afrika
“Kwa sasa Tanzania ni mzalishaji wa pili wa tumbaku Afrika kutoka katika kundi linaloitwa ‘others’ ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani elfu 70.69 mwaka 2021/2022 na sasa ni uzalishaji wa tani 125,592 msimu ujao tunatarajia kufika tani laki 2,” amesem Waziri Bashe
Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo inaweka mikakati ya kuifanya Tanzania kuongoza Africa na Duniani kwenye zao la Tumbaku.