Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa unafuu zaidi wa gharama ya data kati ya Nchi 55 Barani Afrika.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr. Jabir Bakari wakati akizungumza kwenye mjadala kuhusu kuhusu Maendeleo katika Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, katika kipindi cha Mwaka mmoja wa utendaji wa Rais Samia.
Dkt. Jabiri Pia amesema kati ya Nchi 155 Ulimwenguni, Tanzania inashika nafasi ya 21 kwa unafuu wa gharama za kununua GB 1.