Serikali imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri anayeshughulika na masuala ya Wakimbizi Nchini Uganda, kuwa Tanzania inawalazimisha Wakimbizi waliopo katika kambi mbalimbali Nchini kurejea Burundi bila ridhaa yao.
Akizungumza katika warsha ya maandalizi ya uandishi wa kitabu cha historia ya hifadhi ya wakimbizi nchini, iliyofanyika Jijini Arusha, Simbachawene amesema Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi hivyo tuhuma hizo sio sahihi.
“Nimemsikiliza Waziri anayeshughulika na masuala ya wakimbizi wa Uganda katika kipindi cha BBC Dira ya Dunia akiwa anailaumu Tanzania kwamba inawafukuza wakimbizi na kuwalazimisha waingie Uganda, jambo hilo ni tuhuma nzito” Simbachawene
“Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi, Tanzania haijawahi kufanya oparesheni wala shughuli yoyote kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda kuwarejesha au kufanya vyovyote vile” Simbachawene
“Tunamshangaa huyu Waziri mwenzangu wa Uganda amelichukua wapi jambo hilo na kulisema kwenye vyombo vya habari vikubwa linatushangaza na kuonyesha masikitiko yetu na kama kulikuwa na njia nyingine tungewasiliana kwanza kwasababu tunafnaya kazi kwa pamoja kuliko hiki alichokifanya” Simbachawene
“Sisi Tanzania ni wazoefu tumehifadhi sio tu wanaotoka nchi nyingine hata Wauganda wenyewe tuliwahifadhi, sasa leo hii sisi tuliowahifadhi wenyewe tukawe watu wabaya katika ukanda huu” Simbachawene
“Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi kabla ya Uhuru na baada ya uhuru na yote ni kusema nchi hii ina usalama na ulinzi mzuri kwa wakimbizi kwani takribani wapigania uhuru wa nchi za SADC walijihifadhi katika nchi ya Tanzania” Simbachawene
LOWASSA AMUAMBIA RAIS MAGUFULI “INATISHA LAKINI USITISHIKE, UMMA NA DUNIA INAJUA”