Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) huku mikoa kama Dar es laam ,Pwani ,Manyara,Arusha,Njombe,ikitajwa kuwa na uibuaji wa wagojwa wa TB huku Kigoma,Songwe,Simiyu ,Katavi, Kagera,na Visiwa vya Zanzibar ina kiwango cha chini cha uibuaji wa wagojwa wa TB’.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Health Promotion Tanzania (HDT), Dk Peter Bujari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani hapo jana kuwa maambukizi makubwa ya ugonjwa huo katika nchi hizo 30 yanachangia asilimia 87 ya maambukizi yote duniani.
Amesema takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha kuwa, Tanzania ilikuwa na wagonjwa 128,000wa kifua kikuu, na kwamba hadi sasa maambukizi mapya ni 100,000 na wagonjwa 18,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Zaidi ya watu Billioni 2 sawa na asilimia 25 wanaishi na maambukizi ya ugojwa wa kifua kikuu nchini hivi sasa huku makundi hatarishi ya kupata maambukizi yakiwa ni watu wenye magojwa sugu,wavuta sigara ,watu wanaoishi kwenye mazingira duni ,wanaoishi na wenye maambukizi ,wazee,wakimbizi nk.