SERIKALI ya Tanzania imepanga kuingiza kiasi cha dola bilioni 15 za Marekani kupitia uwekezaji kutoka nje (FDI) kufikia mwishoni mwa mwaka 2025.
Taarifa hiyo ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na India lililofanyika New Delhi, India ambako Rais yuko kwenye ziara ya kitaifa ya siku nne.