CPA Faustine Masaru mhasibu Mwandamizi Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), amesema wanahakikisha majukumu yanatendeka kwa ufanisi.
Amesema kupata tuzo hiyo inamanisha kwamba wanafanya kazi kwa usahihi na ufanisi.
Katika hatua nyingine, amesema wanafikiria kutumia meli zisizo na rubani ili kuongeza ufanisi zaidi.
“Sasa hivi kuna mabadiliko mengi ya kiteknoilojia yanatokea ikiwemo meliz hizo zisizo na rubani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhasibu na Fedha Tasac, Pascal Karomba amesema wanahakikisha bahari ina usalama na ulinzi kama ilivyo majukumu yao Tasac.
Amesema uimarishwaji wa usafiri wa majini ndio chachu ya kupata tuzo hiyo.
“Tuzo hii inamaana mdhibiti wa usafiri majini kuhusu usalama na mazingira anasimamia majukumu yake kama ilivyopaswa.”
Amesema wanahakikisha Tanzania inakua mahali salama na penye ufanisi zaidi katika shughuli na biashara za meli.