Pichaz za utoaji wa Tuzo za TASWA 2015 na Rais Jakaya Kikwete akipewa Tuzo ya heshima
Share
4 Min Read
SHARE
Hatimaye lile tukio la utolewaji wa Tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) ambazo hutolewa kila mwaka kwa wanamichezo wanaofanya vizuri, zimekamilika usiku wa October 12 kwa wanamichezo, taasisi na viongozi waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, Tuzo hizo safari hii zimekuwa tofauti na miaka yote kwani waliopewa Tuzo ni wale waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa maalum mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga Rais Kikwete kwa kumaliza muda wake madarakani na kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala wake. Ikumbukwe kuwa Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi iliyochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
Tuzo zimetolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi, viongozi waliochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na Tuzo ya heshima kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis Cheka, Mbwana Samatta, Iddi Kipingu, Abdallah Majura na Hasheem Thabeet
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.