Leo August 30, 2020 kuna hii ya kuifahamu juu Kampuni ya Sky Drive Inc ya nchini Japan imefanikisha jaribio lake la kwanza la kuendesha na kurusha gari linalopaa angani likiwa na mtu mmoja.
Katika video iliyowekwa mtandaoni mwishoni mwa wiki hii, kifaa hicho kinachoonekana kuwa na muundo wa pikipiki lakini kina ‘propellers’, kilipaa umbali wa kati ya mita 1-2 kutoka ardhini, kikifanya safari hiyo kwa dakika nne.
Mkuu wa Kampuni inayotengeneza Tomohiro Fukuzawa amesema kuwa jitihada zao zinawapa matumaini kuwa gari hilo linalopaa linaweza kuwa sio ndoto tena ifikapo mwaka 2023.