Ikiwa ni saa kadhaa toka Rais Samia Suluhu Hassan awasili Dar es salaam akitokea Dubai alikokua na ziara ya kikazi na kuhudhuria Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania ndani ya maonesho ya Dubai Expo, rangi za bendera ya Tanzania zimelipamba jengo maarufu duniani la Burj Khalifa, Dubai.
Jengo hili ndio linalotajwa kuwa jengo refu kuliko yote duniani lina gorofa 163 na lilianza kujengwa January 2004 na likafunguliwa miaka sita baadae January 4, 2010 na hadi sasa limekua moja ya vivutio vikubwa vya kitalii duniani.
Uwepo wa Jukwaa la Tanzania kwenye maonesho ya Dubai EXPO umezaa matunda ya kusainiwa kwa hati 36 za makubaliano zenye thamani ya USD bilioni 7 ambazo ni sawa na Trilioni 17.1 za Tanzania huku ajira zinazotarajiwa kuzalishwa zikiwa ni laki mbili na elfu nne na mia tano sabini na tano.
Sasa hapa nakusogezea ushuhudie wakiwa wameiweka picha ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
FAHAMU MATAIFA TISA YENYE UWEZO MKUBWA WA SILAHA ZA NYUKLIA DUNIANI, URUSI KINARA