Kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe imeahirishwa hadi Agosti 13, 2021 kwa ajili ya Upande wa Mashitaka kuwasilisha taarifa za kesi hiyo kutoka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Hata hivyo, mshtakiwa Mbowe na wenzake watatu wamesomewa upya mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambayo ni kula njama na tuhuma za Ugaidi ambayo waliyatenda kati ya Mei 1 na August 1, 2020 maeneo ya Moshi, Dar es Salaam, Morogoro na Arusha.
Mbowe alifikishwa kwa mara ya kwanza July 26, 2021.
KESI YA UGAIDI: MBOWE ASOMEWA UPYA MASHTAKA, WAKILI ASEMA “ULIPUZI WA VITUO VYA MAFUTA”