Wananchi wa Mtaa wa Kilongo Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro wamefunga barabara ya Morogoro-Dodoma kwa saa kadhaa wakishinikiza Serikali kuweka Alama za barabarani katika eneo hilo baada ya mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkundi kugongwa na gari na kufariki.