Ni Ripoti za utoaji wa huduma ya Chanjo ya kujikinga na Ugonjwa wa (Covid-19) Uviko 19, sasa leo Agosti 3, 2021 Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni imeanza kutoa huduma hiyo kwa Wananchi wake.
Ayo TV & Millardayo.com ilimpata Dkt.Mukiza Ngemera ambae amezungumzia wingi wa watu waliojitokeza siku ya leo kupata chanjo hiyo.
“Tunamshukuru Mungu zoezi limeendelea vizuri tangu siku ya leo kama siku ya kwanza ambapo tumeanza zoezi hili la uchanjaji chanjo dhidi ya virusi vya Corona kiukweli muamko umekuwa mkubwa sana na leo tumeanza saa mbili asubuhi na ni zoezi endelevu”-Dkt Mukiza Ngemera
WATU WANAVYOSUBIRIA CHANJO HADI MUDA HUU ARUSHA “HADI 300, TUMESHINDA NJAA”
ANGALIA RC ARUSHA ALIVYOCHANJWA “NAOGOPA SINDANO, SINA HIARI SIJASIKIA CHOCHOTE”
CHANJO YA UVIKO 19 DODOMA YAANZA KUTOLEWA, TAZAMA ILIVYOKUWA
GUMZO!! MUOSHA MAGARI ALIENDA KUTAMBA NA GARI LA MTEJA APATA NALO AJALI DODOMA