Mwalimu wa hesabu na fizikia kutoka Shule ya Sekondari kwenye kijiji kilichopo eneo la Bonde la ufa Nchini Kenya aitwae Peter Tabichi ameshinda Tuzo ya Mwalimu Bora kwa mwaka 2019 duniani.
DW SWAHILI (www.dw.com/sw/) wameripoti kwamba Peter Tabichi ambaye Waandaaji wa Tuzo hiyo wanasema hujitolea asilimia 80 ya mshahara wake wa mwezi kwa Watu masikini, amepokea tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika siku ya Jumamosi huko Dubai ambayo Mwenyeji wake alikuwa Staa wa filamu kutoka Hollywood, Hugh Jackman.
Baada ya ushindi wa Dola za Kimarekani MILIONI MOJA ambazo ni zaidi ya pesa za Kitanzania BILIONI 2, Tabichi amesema “Kila siku barani Africa tunafungua ukurasa mpya wa maisha, Tuzo hii hainitambui mimi bali inawatambua vijana wa Bara hili. nipo hapa kwa sababu ya kile ambacho Wanafunzi wangu wamefanikiwa katika maisha yao”
“Tuzo hii inawapa wao fursa, inauambia Ulimwengu kwamba wanaweza kufanya kitu chochote” aliongeza kwa kusema hayo Mwalimu huyo baada ya kuwashinda Walimu wengine tisa kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao waliingia nae pamoja kwenye fainali kuwania tuzo hiyo.
Habari kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani DW >>> BONYEZA HAPA
VIDEO: FURAHA YA RAIS MAGUFULI BAADA YA TAIFA STARS KUSHINDA 3-0, ASEMA “LEO NDIO NIMEONA MPIRA SIO ULE WA SIKU ILE” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA MWANZOMWISHO