Lile tukio la ajabu ambalo limestaajabisha wengi la mti ambao ulikuwa umeanguka kwa zaidi ya miaka mitatu kuinuka, leo limekaa kwenye headline tena ambapo viongozi wa Serikali wamezungumzia hilo huku wananchi wakisisitizwa kuutunza.
Mti huo umeinuka siku ya Oktoba 15 mwaka huu, ambapo Katibu tawala wa Wilaya ya Uyuwi amesema; “…kwa mazingira tunayoyaona hapa tukio ni kweli limetokea sasa ni kwa nguvu zipi kwa uwezo wa Mungu au nguvu za giza hili nadhani kwa sasa litakuwa hatuwezi kulitolea taarifa ,lakini cha msingi eneo hili tulitunze kwa matumizi ya kumbumbuku ya vizazi vyetu na pamoja na wengine watakaotoka nje ya eneo hili, ambao watataka kuja kuona maajabu ya Mwenyezi Mungu tofauti na kule Mfuto ulipoinuka tu siku ya pili yake tukakuta kila kitu hakuna, kwa hiyo nilikuwa napenda niwapongeze Wanakijiji kwa kulinda Mti huu…”
Shuhuda wa kwanza kuzungumzia tukio hilo amesema; “… Haya magome ya mzizi yakichimbwa, yakisagwa mtoto akiwa anaumwa Degedege wakimvutisha ile hali ya mchango inashuka hata kama unaumwa kipanda uso, hata kama unaumwa kichwa cha kawaida…”
Mwanakijiji mwingine amesema; “…Huu Mti kama mbwa wako sio mkali unachimba mizizi unakoboa magome unatwanga ule unga wake unamnusisha kwenye pua anakuwa mkali sana…“
Mtu mwingine amesema; “Kama kuna Mtu ambaye pengine kashaishiwa pengine fahamu wanajaribu kumuwekea puani na mara anapiga chafya…”
Kuisikiliza taarifa iliyoripotiwa na TBC 1 bonyeza play hapa chini.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook