Lionel Messi ni mmoja kati ya wachezaji wa viwango vya Dunia lakini sifa ya kipekee aliowahi kuipata ni kuweka rekodi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara nne, hii ikiwa ni rekodi ya kipekee kwa staa huyo wa FC Barcelona ya Hispania, Alhamisi ya November 12 naomba nikusogezee TBT pichaz zake za utoto ambazo hadi FC Barcelona wanamsajili alikuwa anatajwa kuwa na tatizo la ukuaji.
Staa huyo wa FC Barcelona alianza kucheza soka akiwa na miaka minne katika klabu ya Grandoli, mtu wa kwanza kuchangia kumuhamasisha Lionel Messi kucheza soka katika enzi zake za utoto ni bibi yake Celia ambaye alifariki kabla ya Lionel Messi hajatimiza miaka 11. Kifo hicho kilimuathiri Messi hadi leo hii, ndio maana akifunga goli huwa ananyoosha vidole vyake viwili juu na kufanya ishara ya msalaba, kitu ambacho kinatajwa kama ishara ya kumkumbuka bibi yake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.