Kama kawaida mtu wangu wa nguvu kila siku ya Alhamisi huwa nakuletea TBT, yaani pichaz za wakali wako wa soka hususani picha zao wakati wapo vijana wadogo au watoto, najua umezoea kuwaona wakiwa uwanjani na kuona picha kadhaa za ukubwani.
Ni mara chache sana kukuta mtu ana picha zake nyingi za utoto kwani huwa inaaminika zamani ilikuwa ngumu kuzitunza picha hizo na kufanya zikae kwa miaka mingi hususani katika wakati ambao hakuna mitandao ya kijamii kama sasa hivi kitu ambacho husaidia kutunza kumbukumbu ya picha zako.
Zlatan Ibrahimovic huyu ni moja kati ya vijana wa kizungu waliokuwa wanajituma katika harakati za maisha toka yupo mdogo kwani aliwahi kulipotiwa kufanya kazi wakati akiwa na umri mdogo kitu ambacho kilitaka kuchangia kuachana na soka kwa staa huyo kwani alikata tamaa kutoka katika soka.
Cesc Fabregas amekulia katika Academy ya Mataró kabla ya mwaka 1997 kuamua kuhamia katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania. Staa huyu kwa sasa anacheza katika klabu ya Chelsea ya Uingereza. Staa huyo wa Chelsea anayependelea kuvaa jezi namba 4 ana mtoto wa kike anayeitwa Lia.
Yaya Toure ni moja kati ya wachezaji wa kiafrika wanaoiwakilisha vyema Ivory Coast katika bara la Ulaya na kwingineko duniani, Yaya Toure ambaye kaka yake wa damu Kolo Toure aliwahi kuchezea Arsenal kwa mafanikio lakini Yaya kuna wakati aliwahi kufeli majaribio katika klabu ya Arsenal. Yaya ni moja kati ya wachezaji wa Afrika waliotokea maisha magumu kwani alikuwa akicheza soka bila kuvaa viatu.
Memphis Depay mshambuliaji wa Man United aliyesajiliwa katika kipindi cha usajili cha mwezi August 2015 akitokea klabu ya PSV Endhoven ya Uholanzi. Hizi ni TBT pichaz za mkali huyu wa soka ambaye amegoma kutumia jina la Depay katika jezi yake kutokana na baba yake kumuacha na mama yake wakati yupo mdogo hivyo huwa haoni umuhimu wa kutumia jina la baba yake katika jezi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.