Tumezoea kuona siku ya Alhamisi watu wengi hutumia siku hii kuweka TBT pichaz zao katika mitandao ya kijamii, mtu wangu wa nguvu kila wiki nimekuwa nikikuwekea TBT pichaz za mastaa kadhaa wa soka wa nje ya Tanzania hususani Ulaya, picha ambazo zinaonesha muonekano wao wa enzi zao za utoto. Alhamisi ya October 29 naomba nikusogezee karibu yako TBT pichaz za wakali wa soka Tanzania kama Himid Mao, Jerson Tegete, Haruna Chanongo, Athumani Iddi Chuji, Peter Manyika Junior na Said Hamisi Ndemla.
1- Himid Mao ni mchezaji wa klabu ya Azam FC kwa sasa lakini ni moja kati ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwasa.
2- Haruna Chanongo huyu aliwahi kucheza Simba kwa muda kidogo kabla ya kuamua kutimkia klabu ya Stand United ya Shinyanga ambayo anaichezea hadi hivi sasa. Hii TBT picha yake mtu wangu.
3- Athumani Iddi Chuji amecheza timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa muda mrefu hususani katika kipindi cha kocha Marcio Maximo, ni moja kati ya wachezaji walioipeleka Tanzania kushiriki michuano ya CHAN iliyofanyika nchini Ivory Coast michuano ambayo ndio ilisababisha kukorofishana na mwalimu Maximo. Chuji kwa sasa yupo Mwadui FC
4- Jerson Tegete ni moja kati ya wachezaji waliowahi kufanya vizuri katika timu ya taifa ya Tanzania enzi za kocha wa kibrazil Marcio Maximo, Tegete jina lake lilianza kung’aa wakati akiwa shule ya Sekondary ya Makongo wakati ambao ilikuwa ikisimamiwa na Iddi Kipingu. Tegete kwa sasa anacheza Mwadui FC ya Shinyanga baada ya kuachwa na Yanga.
5- Said Hamisi Ndemla ni miongoni mwa vijana wanaocheza timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba ambayo inaongoza kuwa na wachezaji vijana zaidi, Ndemla anajulikana kwa uwezo wake wa kupenda kupiga mashuti akiwa nje ya eneo la 18.
6- Peter Manyika Junior huyu haishangazi kumuona akifanya vizuri golini kwa sababu ni moja kati ya magolikipa waliorithi vipaji kutoka kwa baba zao, Manyika Senior ambaye ni baba mzazi wa Manyika Junior aliwahi kuwa golikipa wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania. Manyika Junior kwa sasa yupo Simba.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.