Binadamu hupitia hatua nyingi hadi kuja kufikia mafanikio, wengi wamepata shida katika harakati za kusaka mafanikio, huenda umewahi kuwaona mastaa kadhaa wa soka wakiwa na mafanikio na hukuwahi kuwaona wakiwa katika muonekano wao wakati wapo wadogo. Ninayo list ya TBT pichaz ya mastaa wa soka.
1- Robin van Persie amewahi kucheza katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kabla ya mwaka 2012 kuhamia Man United, alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Excelsior mwaka 1997 na mwaka 2001 akaanza kuchezea timu ya wakubwa ya Feyenoord na sasa anakipiga katika klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki. Hizi ni TBT Pichaz zake mtu wangu.



2- Santi Cazorla ni kiungo wa kimataifa wa Hispania aliyezaliwa 13 December 1984 Llanera Hispania kwa sasa anakipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza, alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Covadonga mwaka 1992 ila mwaka 2003 hadi 2006 ndio alianza kutambulika rasmi katika ulimwengu wa soka akiwa na klabu ya Villarreal. Nimekutana na picha yake ya utoto.


3- Pedro Rodriguez maisha yake ya soka alianzia katika klabu ya San Isidro na baadae FC Barcelona kabla ya 2015 kuamua kuhamia Chelsea kutokana na kuwasili kwa Luis Suarez FC Barcelona na nafasi yake ya kucheza kuwa finyu.


4- Alexis Sanchez anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye stamina, alizaliwa Tocopilla Chile na kuanza kucheza soka la vijana akiwa na umri wa mika 16 katika timu ya vijana ya Cobreloa, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza.


Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.