Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekanusha kuinyima kibali Helikopta iliyokuwa itumike na mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu katika mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo na mamlaka hiyo, imesema kuwa Helikopta hiyo imepewa kibali cha muda mrefu (block permit) na TCAA kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 31, 2020 na kukanusha madai hayo.
Mkurugenzi Mkuu TCCA, Hamza Johari amekanusha pia uwepo wa ofisa wa mamlaka hiyo aliyetoa taarifa kuhusu safari ya msafara wa Mhe. Lissu kutokuwepo kwani safari ya CHADEMA haikuwepo kwenye orodha.