Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji Leseni za Maudhui Mtandaoni kuanzia Januari 28 hadi Juni 30 2021.
Hayo yamebainishwa na Mhandisi Francis Mihayo, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa alipokuwa katika Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa.
TCRA imesema hatua ya kusitisha utoaji leseni kwa ‘Blogs’ na ‘Online TV’ inatokana na kuendelea kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa matumizi sahihi ya mtandao.
Katika kipindi hicho ambacho hawatatoa leseni watakuwa wanafanya tathmini ili kutoa fursa za kurekebisha dosari zilizojitokeza.
Via: HabariLEO