Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imesema, Vituo vya Utangazaji ambavyo vitarusha matangazo mubashara vinaelekezwa kufuata mwongozo ili kuwa na ufanisi katika usimamizi na ufuatiliaji wake.
Imesema, kituo kitakachorusha matangazo mubashara kama vile Sherehe za Kitaifa ambazo ziko kwenye kalenda kinapaswa kutoa taarifa siku 14 kabla, taarifa hiyo itaeleza mahali, muda wa kuanza na kumaliza tukio.