Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mfumo wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole (Biometric). Mfumo huo umezinduliwa leo March 1, 2018 na utatumika kuhakiki taarifa za wateja wapya wa kampuni zote za simu Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Engineer James Mitayakingi hatua hiyo imetokana na changamoto wanazokumbana nazo katika usimamiaji wa huduma hiyo.
“Kutokana na changamaoto hizo na kuongezeka kwa watumiaji wa huduma hii kuna umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za watumiaji kwa ajili ya matumizi ya usimamizi, kiuchumi na kiusalama,” –Engineer James Mitayakingi
MAAMUZI: SIKU 100 TOKA MWANDISHI WA MWANANCHI ACHUKULIWE NA WASIOJULIKANA