March 8, 2018 ni maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo leo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kwa mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa.
Katika hotuba yake Dr Tulia alisema “Kwanza katika kuitambua siku hii kuwa muhimu Rais Dkt John Pombe Magufuli ametoa salamu za pongezi kwa wanawake wote duniani katika kutambua mchango wetu katika kujenga ustawi wa jamii”
“Tunaposherekea sherehe hii kama wanawake tunataka kusherekea kwa yale mazuri tuliyofanikiwa katika kuboresha jamii yetu lakini pia tukumbushane yale yaliyopo katika jamii ambayo yanatukandamiza. Sisi wakinamama hatutarajii kuendelea kuwa hapa tulipo, kila tunachokifanya lazima tukifanye kwa ubora na utofauti na wengine wanavyo fanya ili kufikia lengo”-Dr Tulia
Kauli ya Dr Tulia baada ya kuambiwa hatimizi ahadi