Mwaka 2016 umekuwa ni mwaka ambao watengenezaji wa simu nyingi wamejaribu kufidia kigezo cha kuwa na betri inayodumu ikiwa imetengenezwa na teknolojia inayoipa uwezo wa kuchaji kwa haraka zaidi na kubaki kwa muda mrefu. Watengenezaji wa simu ya smartphone aina ya Phantom 6+ wametumia utaalamu wa hali ya juu katika kutengeneza betri inayodumu kwa muda mrefu zaidi.
Unaambiwa TECNO Phantom 6+ ina uwezo wa kuchaji kwa haraka zaidi, kutokana na MediaTek Helio x20 yenye mfumo wa deca-core ambayo ipo kwenye TECNO Phantom 6+ itakayozinduliwa hivi karibuni, teknolojia iliyotumika inaipa betri ya simu hiyo nguvu kwa muda mrefu.
Awali, katika majaribio yaliyofanyika na wachambuzi wa teknolojia, TECNO Phantom 6+ ilibainika kuwa ikiwa haina chaji (0%) inaweza kujaa mpaka asilimia 35% ndani ya dakika kumi (10%) tu!
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 16 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI