Mwezi mmoja tangu kufariki kwa mgonjwa wa kwanza aliyegundulika kuwa na maambukizi ya Ebola Marekani, ndugu wa mtu huyo wametoa shutuma kali kuhusiana na kifo cha ndugu yao.
Maswali ni mengi ambayo yamepelekea hasira kwa ndugu wa mtu huyo Thomas Eric Duncan wakiwa wanahoji; “..kama watu wengine wameumwa Ebola wakiwa ndani ya Marekani na wamepona imekuwaje ndugu yao akafariki?..”
Dada wa mtu huyo, Mary Pearson amesema; “.. Eric ameteseka akiwa mbali na mimi, naumia sana.. Hawakumuonea huruma.. Hawakumpatia dawa.. Walikuwa na uwezo wa kumtibu lakini walimhudumia kama mbwa. Ni waovu.. Hawakumtibu kwa kuwa walisema yeye ndiye aliyepeleka Ebola ndani ya Marekani..”
Familia ya Duncan ilifungua mashtaka dhidi ya Hospitali ya Texas Health Presbyterian kwa uzembe uliopelekea mauti ya ndugu yao kwa kuwa alifika Hospitali akiwa na dalili za awali lakini hawakujali kumtibu, badala yake walimpatia dawa za kupunguza maumivu na kumrudisha nyumbani.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook