Upendeleo wa Erik ten Hag ni kuendelea kuitumikia Manchester United msimu ujao licha ya Bayern Munich kufanya mawasiliano kuhusu nafasi ya meneja aliyeachwa wazi.
Bayern wanatafuta meneja mpya baada ya kutangaza Februari kuwa wataachana na Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu.
Juhudi za kuwarubuni Xabi Alonso, Julian Nagelsmann na Ralf Rangnick zimeambulia patupu, na kupelekea upande wa Ujerumani kutathmini wagombea wengine.
Chanzo kimoja kimeiambia ESPN kwamba kumekuwa na mawasiliano kati ya Bayern na wawakilishi wa Ten Hag katika juhudi za kuelewa msimamo wa Mholanzi huyo.
Kuna kukubalika kwamba kibarua cha Ten Hag huko United kiko hatarini baada ya msimu mbaya, lakini Bayern wameambiwa kwamba anachopendelea ni kubaki Old Trafford.
Ten Hag ana mkataba katika klabu hiyo hadi 2025, ingawa hajapewa hakikisho rasmi na mmiliki mwenza mpya Sir Jim Ratcliffe kwamba bado atakuwa meneja mwanzoni mwa msimu ujao.
Ratcliffe na timu yake ya usimamizi ya Sir Dave Brailsford, Mkurugenzi Mtendaji wa muda Jean-Claude Blanc na mkurugenzi mpya wa kiufundi wanafikiria wagombea wengine wa jukumu hilo, akiwemo Tuchel.