Shirikisho la soka duniani FIFA liliingia kwenye headlines baada ya viongozi wake kukumbwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha.
Sasa ni zamu ya mchezo wa tennis baada ya uchunguzi kubaini kuwepo udanganyifu wa kupanga matokeo ya mechi katika mashindano mbalimbali ya tenisi duniani ikiwemo shindano la Wimbledon.
Nyaraka za siri zimeonyesha kuwa katika miaka 10 uliopita wachezaji 16 waliokuwa kwenye nafasi 50 za juu wametambuliwa na maafisa wanaosimamia mchezo huo kwa hofu ya kukubali kushindwa kwa hiari tangu mwaka 2007.
Idara ya kupambana na ufisadi ya mchezo huo imesema imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya dalili zozote za kupanga matokeo na ufisadi unaohusiana na mchezo wa kamari.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.