Akiwa na mkataba na Paris Saint-Germain kwa msimu ujao, taarifa za sasa ni kwamba Mbappe ameamua kutoongeza mkataba wake msimu huu wa joto,hivyo, PSG wanataka kumuuza, ikiwa hataongeza mkataba wake huku Real Madrid wakisubiri kwenye endapo dili rahisi litapatikana.
Kulingana na L’Equipe, kama ilivyonukuliwa na Cadena SER, mtazamo wa PSG unatokana na ahadi ambayo Mbappe aliitoa kwa kilabu kwamba hataiacha bure kwa hivyo, wanatarajia ushirikiano katika suala hilo.
kilichoongezwa ni kwamba walikuwa wamekubali kumuuza Mbappe msimu huu wa joto au ujao ili kusafisha hali yao ya Kifedha na UEFA.
Ripoti za awali zilidai kuwa sehemu ya msingi katika mazungumzo ya kuhama ni bonasi ya uaminifu ya €90m ambayo Mbappe alipaswa kulipwa mnamo Septemba.
Mbappe hataki kuachilia ada hiyo, lakini inaeleweka kuwa PSG haiko tayari kulipa ikiwa hayupo, na pia Real Madrid hawako tayari kubeba gharama hizo, na hivyo kuyumba kwa hali hiyo.