Carlos Tevez amerejea katika klabu yake ya zamani ya Boca Juniors iliopo nchini kwao Argentina baada ya kutumia miaka 11 kucheza soka barani Ulaya… Tevez amepokelewa kishujaa na mashabiki na viongozi wa klabu hiyo katika utambulisho rasmi wa kurejea Klabuni hapo.
Nyota huyo wa Argentina aliyetumia zaidi ya miaka kumi kucheza soka barani Ulaya katika vilabu mbalimbali ikiwemo Manchester United, Manchester City na Juventus ametambulishwa mbele ya mashabiki katika Uwanja wa Bombonera Stadium ambao unatumiwa na klabu hiyo kama Uwanja wa nyumbani.
Carlos Tevez ameichezea Boca Juniors kuanzia mwaka 2001 hadi 2004 na kutimkia klabu ya Corinthians ya Brazil na baadae akaelekea zake Ulaya. Tevez pia amecheza mechi 72 na timu ya taifa ya Argentina na kuifungia mabao 13, amecheza kombe la dunia mwaka 2006 na 2010 lakini pia amewahi kutwaa medali ya dhahabu ya Olympic mwaka 2004.
Ada ya uhamisho kutoka Juventus kwenda Boca Juniors haijatajwa na Klabu hiyo lakini vyombo vingi vya habari barani Ulaya vinataja kufikia pound milioni 4.6.
Nimekuwekea video ya utambulisho wa Tevez hapa mtu wangu.
https://youtu.be/R0SaHG4ljrI
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.