October 28, 2016 Nimeipata taarifa ya kukamatwa Dawa bandia za Malaria na Vijiuasumu (Antibiotic) zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 17 na Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA, ambayo imewataka watoa huduma za afya na wafanyabiashara za dawa nchini kuzirudisha TFDA kabla hawajachukuliwa hatua kali zaidi.
Imeelezwa kuwa Dawa hizo zimegundulika baada ya zoezi la ukaguzi lililofanywa na mamlaka hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, ametaja baadhi ya dawa zilizokamatwa katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Mara, Geita na Shinyanga kuwa ni vidonge vya aina ya Eloquine, Quinine Sulphate ambazo hutibu Malaria, Erythromicin, Doxycyline na Siproflaxine ambazo hutumika kama Viuajisumu.
Aidha Hiiti Sillo amesema uchunguzi wa awali umeonesha kwamba dawa hizo bandia zinatengenezwa hapa nchini katika makazi ya watu na maeneo mengine ya kificho ambapo dawa zilizoisha muda wa matumizi pia huongezwa muda kwa kuondoa alama za zamani na kubandika mpya na kishwa kuuzwa madukani kwa wagonjwa.
ULIPITWA NA MAAMUZI YA BENKI KUU YA TANZANIA BOT KUIWEKA CHINI YAKE BENKI YA TWIGA BANCORP? TAZAMA HAPA