Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uturuki (TFF) Mehmet Buyukeksi ametangaza kusimamisha kwa muda usiojulikana michezo yote ya Ligi zote nchini humo kufuatia shambulizi la muamuzi Halil Umut Meler wa mchezo wa sare ya 1-1 wa Ligi Kuu Uturuki kati ya MKE Ankaragucu dhidi ya Rizespor.
Shambulio kwa muamuzi huyo lilianza pale Rais wa timu ya Ankaragucu, Faruk Koca kumpiga ngumi refa Halil Umut Meller baada ya mchezo kupelekea watu wengine kumshambulia zaidi kiasi cha kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Faruk Koca hakuoneshwa kuridhishwa na uamuzi wa refa huyo ambao ulipelekea timu pinzani Rizespor kusawazisha bao dakika ya 97 ya mchezo na kuisha 1-1.