Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF pamoja na afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura wametangaza September 9 kuingia katika makubaliano ya udhamini na mfuko wa Bima ya afya kwa ajili ya wachezaji wa Ligi Kuu na viongozi.
TFF wamethibitisha mpango huo, mkataba watasaini hivi karibuni kwani unadhumuni la kulinda afya za wachezaji, kupitia kwa msemaji wa mfuko wa Bima wa taifa Singu amethibitisha mpango huo wa kuingia mkataba wa udhamini kwa vilabu vyote 16 vitakavyoshiriki Ligi Kuu.
Mpango huo ni kuwa wachezaji 30 wa Ligi Kuu na viongozi saba ambao wapo klabu moja watapata nafasi ya kupata kadi ya Bima ya afya bure bila kuchangia chochote, hii ni kutokana na mkataba huo wa udhamini utakaosainiwa na TFF kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos