Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kupitia kamati ya haki na hadhi za wachezaji December 23 ilikaa na kupitia mapingamizi yalikuwa yamewasilishwa kuhusu suala la usajili, mara tu dirisha dogo la usajili lilipofungwa December 15 mwaka huu.
Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Richard Sinamtwa imekaa December 23 na kupitia usajili wa vilabu mbalimbali na kupisha usajili wa baadhi ya wachezaji ila imezuia pia usajili wa baadhi ya wachezaji kutokana na kuwa na mapungufu ambayo hayakukamilishwa katika usajili. Kamati hiyo pia imezuia usajili wa Danny Mrwanda na Lulanga Mapunda hadi Lipuli FC na Maji Maji FC taarifa ya maandishi kuhusu kukubaliana kwa usajili wa wachezaji hao.
Ifuatayo ni ripoti kamili ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji
A. USAJILI
- Kamati imepitisha usajili wa wachezaji walioombewa kwa vilabu vifuatavyo vya ligi kuu
-
AZAM FC – mchezaji mmoja Ivo Philiph Mapunda (huru)
- COASTAL UNION – wachezaji watatu
i. Omary Wayne Maunda-Mkopo toka Azam FC
ii. Miraji Adam Seleman-mkopo toka Simba
iii. Ramadhani Ali Thabit-huru
- MGAMBO SHOOTING
i. Mudathir M. Khamis–Yanga
ii. Nurdin Mkomeni-huru
iii. Godson Mmasa-alikuwa mchezaji wa Mgambo, wameomba kumsajili tena
4. MTIBWA SUGAR
i. Alex Mwambisi-huru
ii. Boniface Maganga-Mkopo kutoka Simba
iii. Kelvin Iddi Friday-Mkopo kutoka Azam FC
iv. Abdallah Said Makangana-alisahaulika usajili uliopita ni mchezaji anayendelea
- MWADUI SC
i. Abdallah Mfuko-huru
ii. Ismail Gambo -Mkopo kutoka Azam FC
6. NDANDA SC
i. Braison Raphael-Mkopo kutoka Azam FC
ii. Jackson John Nkwera-Sinza Srtars
7. MBEYA CITY
i. Ramadhani Selemani Chombo-huru
ii. Abdallah Salum Juma-Toto Africans
iii. Deogratius Julius–Kagera Sugar
8. TANZANIA PRISONS
i. Baraka Majogoro–Wenda FC
9. TOTO AFRICANS
i. Shija Hassan Mkina-huru
ii. Frank B Kimati-huru
iii. Ladslaus Mbogo-huru
iv. Yusuf Seleman Mpili-huru
v. Maneno Steven Shaban-huru
- SIMBA SC
i. Kiongera Raphael-Amerudishwa toka KCB alikokuwa anacheza kwa mkopo
ii. Novaty Lufunga–African Sports
iii. Haji Mohamed Ugando–Jaki Academy
iv. Brian Majegwa–Azam FC
- STAND UNITED
i. Assouman N’gueassan David–FC Olympic Sports Abobo
- YOUNG AFRICANS
i. Issoufou Boubacar–
ii. Paul Nonga–Mwadui FC
- JKT RUVU
i. Waziri Shaban Iddi-huru
ii. Hamis Thabit–African Lyon
iii. Hassan Dilunga–Stand United
- MAJI MAJI FC
i. Kennedy Stainley Kipepe–Njombe Mji
ii. Abubakar B Bakari-huru
iii. Sixmund Ally Mwakasekaga-huru
iv. Paulo Maona Terry-huru
- KAGERA SUGAR
i. Ramadhani Mzee Kipalamoto–Kagera Sugar
ii. Samwel Donald Ngassa-huru
iii. Shaaban Ibrahim Sunza–Mshikamano
iv. Martin Lupart Mlolere–Abajalo, Dar es Salaam
v. Juma Jabu Hamis-huru
- AFRICAN SPORTS
i. Hamis Twairu Juma-U20, huru
ii. Hamad Nathaniel Mbumba–Polisi Tabora
iii. Hamad Nathaniel Mbumba–African Lyon
iv. Charles Martin Ilamfya-Mkopo toka Mtibwa
v. Rajab Isihaka-huru
vi. Reyna Mgungira-huru
USAJILI UFUATAO UMEZUILIWA KWA MAELEZO YAFUATAYYO
- AFRICAN SPORTS
i. Karim Hamud Juma aliyeombea kusajiliwa na African Sports akitokea Polisi Tabora usajili wake
ii. Michael Victor Mgimwa kamati imezuia usajili wake mpaka hati ya uhamisho wa kimataifa umezuiwa mpaka timu mbili zitakapofikia makubaliano itakapotumwa toka Thailand, mchezaji huyu alikuwa anaitumikia Rio United ya Thailand.
- MAJI MAJI FC
i. Danny David Mrwanda na Lulanga Andrew Mapunda-kamati imezuia usajili wake mpaka vilabu viwili vya Majimaji inayotaka kumsajili na Lipuli iliyokuwa inawamiliki wachezaji hao zitakapokubaliana na kutuma kwa maandishi makubaliano yao TFF.
3. MBEYA CITY
i. Kamati baada ya uchunguzi imejiridhisha kwamba mchezaji Tumba Sued aliyewekewa pingamizi na Coastal Union alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Coastal Union siku ya tarehe 12 June, 2014 na mkataba huu ulienda kushuhudiwa kwa mwanasheria siku ya tarehe 23 Agosti 2014, kushuhudiwa huku hakukubatilisha mkataba uliosainiwa tarehe 12 June 2014.
Hivyo kamati inamtangaza Tumba Sued kuwa mchezaji huru toka tarehe 11 Desemba na kwa sasa ni mchezaji halali na amepitishwa kuichezea Mbeya City ya Mbeya.
ii. Kamati pia inatoa onyo kali kwa klabu ya Mbeya City na imeagiza kesi hii ipelekwe kwenye kamati ya nidhamu kwa kuongea na mchezaji Ditram Nchimbi ambaye ni mchezaji halali wa Majimaji ya Songea ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili na Maji Maji tarehe 20 Oktoba 2014 hivyo mkataba wake utaisha tarehe 19 Octoba 2016. Mbeya City wameongea na mchezaji mwenye mkataba uliozidi miezi 6 bila kuomba ridhaa ya klabu inayommiliki ambayo ni Majimaji.
- JKT RUVU
JKT Ruvu iliomba kumsajili mchezaji Hassan Dilunga kutoka Stand United kwa kufata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuongea na klabu yake ya Stand United na kupata kibali cha kumsajili Dilunga kutoka kwa uongozi halali wa Stand United kupitia kwa mwenyekiti na katibu wa Stand United. Pamoja na ruhusa kutoka kwa Stand United bado kuna mtu anayeitwa mratibu wa Stand United aliiandikia barua TFF akipinga usajili wa mchezaji huyu.
Kamati imesikitishwa na kiendo cha mtu huyu ambaye hatambuliki na TFF na wala siyo mtu anayepaswa kuwasiliana na TFF kwa kuingilia maamuzi ya viongozi halali wa Stand United na imeamuru mtu huyo anayeitwa Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kwa kupora mawasiliano ya Stand United wakati viongozi halali wanaotambulika kikatiba wa Stand United wapo.
Kamati imeamua mratibu Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kufuatia kutofata na kuheshimu uongozi halali wa klabu ya Stand United.
- NDANDA SC-RAMADHANI KIPALAMOTO
Klabu ya Ndanda SC ilileta maombi ya kumsajili mchezaji Ramadhani Salim Kipalamoto amabye alikuwa anachezea Abajalo SC ya Dar es Salaam, maombi haya yamekataliwa kwa kuwa mchezaji husika alikuwa pia ameombewa kusajiliwa na Kagera Sugar na klabu yake ya Abajalo ikatoa ridhaa ya mchezaji huyu kwenda Kagera Sugar ya Kagera.
- NDANDA SC-IBRAHIM IS-HAAK
Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji imeridhia ombi la mchezaji Ibrahim Is-haki aliyedai klabu yake ya Ndanda SC kuvunja mkataba wake kwa kutomlipa hela yake ya usajili kama walivyokubaliana.
Mchezaji huyu amevunja mkataba wake baada ya maombi yake TFF kukubaliwa na mwakilishi wa klabu yake ya Ndanda SC, Edmund Njowoke ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Ndanda SC, na kamati imeridhia maombi ya timu ya Geita SC ya kutaka kumsajili.
Mchezaji Ibrahim Is-haaka amepitishwa kuichezea timu ya Geita Gold SC ya Geita.
- MWADUI FC
Kamati imeridhia pingamizi la klabu ya KMC ya Kinondoni kumzuia mchezaji Emmanuel Memba aliyeombewa kusajiliwa na Mwadui FC kwa kutofata utaratibu. Kamati inaiagiza klabu ya Mwadui kuongea na KMC wamiliki wa mchezaji ili wawaruhusu kumtumia mchezaji husika.
8. KIMONDO SC
Klabu ya Kurugenzi ya Mafinga imeleta pingamizi dhidi ya Kimondo FC kwa kumsajili mchezaji wao George Mpole bila kufata utaratibu. Kamati inaishauri Kimondo SC kufata utaratibu wa usajili kwa kuongea na Kurugenzi.
- GEITA GOLD SC
TFF imepokea ombi la pingamizi kutoka kwa timu ya Rhino Rangers kwa Geita Gold SC kumsajili mchezaji wao Pius Kisambale bila kufuata utaratibu. Geita inatakiwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kuongea na uongozi wa timu ya Rhino SC ya Tabora
- POLISI MOROGORO
Imeleta ombi la pingamizi la wachezaji wao wawili
i. Anafi Selemani Ally
ii. Mohamed Kapeta kusajiliwa na timu yoyote kwa kuwa ni wachezaji wao. Ombi la pingamizi kwa wachezaji hao limekubaliwa na kamati
CHANZO CHA HII STORI: tff.or.tz
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.